Bei Yako Mbona Kubwa Sana?

Bei Yako Mbona Kubwa Sana?

Ushawahi kukutana na hilo swali pale unapomtajia bei mteja wako?

Miongoni mwa wauzaji wengi huwa wanashindwa kujua wajibu vipi, wengi hufikiria njia ya kutatua hilo ni kupunguza bei lakini wengine wao hukata tamaa kabisa na kuhisi huyo sio mteja wake.

Lakini ukweli ni kwamba, kikwazo hiko ni sehemu tu ya mchakato wa mauzo ambao mteja hupitia, kununua au kutonunua itategemea na wewe unakabilije kikwazo hiko. Nami nitakwambia njia sahihi ya kukabiliana nacho.

Mtu akikwambia bei yako kubwa sana maana yake ni kwamba ameona thamani ya bidhaa yako na bei haziendani hivyo unachotakiwa ni kuelezea zaidi vipengele/sifa zilizopo kwenye bidhaa yako ambazo zinaifanya kuwa bora ukilinganisha na za watu wengine. 

Muelezee kitu gani cha utofauti ambacho kinapatikana lakini kwa watu wengine hakipatikani kabisa au hakipatikani katika ubora kama wako.

Kwa, mfano unaweza kumwambia ukinunua hii kwangu unapata warranty ya miezi 12 lakini kwa wengine huwa ni miezi sita tu, kwahiyo kwangu usalama wa bidhaa yako ni mkubwa.

Lakini pia kama atakuwa hajaelewa unaweza kumpa machaguo mengine ambayo yanaendana na bajeti yake. Kama alitaka manukato ya Tsh 50,000/= na akaiona bei kubwa mwambie yapo mengine ambayo ni Tsh 10,000/= lakini ubora wake ni tofauti (unaweza mpa sababu)

Pamoja na hayo yote, hakikisha unaweka bei rafiki zinazoendana na soko lako (fanya utafiti kwa washindani wako)

Tunahitaji kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

www.instagram.com/oasis_tech_tz

www.oasistech.co.tz

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for