Kukatika kwa huduma ya twitter kumezua sitofahamu kwa watumiaje wake. 😰😱

Kukatika kwa huduma ya twitter kumezua sitofahamu kwa watumiaje wake. 😰😱

Kukatika kwa huduma ya Twitter kunawafanya watumiaji kuambiwa kuwa “wamevuka kikomo cha ku-tweet kwa siku”

Baadhi ya watumiaji wa Twitter hawakuweza kutweet Jumatano baada ya tovuti hiyo kupata matatizo ya kiufundi.

Thursday, February 9, 2023

Wamiliki wa akaunti walipokea ujumbe unaosema: "Umevuka kikomo cha kila siku cha kutuma Tweets." Tovuti ya kufuatilia kukatika kwa mitandao ya DownDetector iliripoti hitilafu hiyo kabla ya saa 22:00 GMT.

Elon Musk amepunguza wafanyakazi wa Twitter miezi michache iliyopita tangu aliponunua jukwaa hilo Oktoba mwaka jana kwa $44bn (TZS 103 Tril).

Mwezi uliopita bosi wa Tesla na SpaceX alisema Twitter ilikuwa na wafanyakazi wapatao 2,300 - kutoka takriban 8,000 alipochukua nafasi ya ukurugenzi.

Kwa miezi kadhaa wataalam wamekuwa wakionya kwamba upunguzaji mkubwa kama huo unaweza kusababisha maswala ya kiufundi, ingawa bado haijabainika ikiwa kupunguzwa kwa idadi ya watu ndio chanzo cha katiko(sumbuko) la kimfumo la Jumatano.

Inaonekana sehemu iliyokuwa na itilafu ilirekebishwa hivi karibuni, na watumiaji wengi wakiripoti kuwa wanaweza ku-tweet.

Wengine waliripoti kuarifiwa na Twitter kwamba walikuwa wamevuka kikomo cha tweet-2,400 kwa siku, japo kuwa hawakuchapisha(tweet) kabisa Jumatano. Inaonekana mifumo imeratibiwa vibaya, na kutoa taarifa za uongo kwa watumiaji? – Nani wakupewa lawama hii? Itilafu hii imeletwa na upungufu wa nguvu kazi? Yote ni maswali yanayohitaji majibu yakinifu.

Wamiliki wa akaunti pia wameripoti matatizo wanayokutana nayo wakitaka kutumia kitufe cha kutuma jumbe(messages) kupitia Twitter. Watumiaji kadhaa walisema hawakufanikiwa pia kutumia TweetDeck - dashibodi ambayo inaweza kutumika na Twitter.

Bado haijabainika ni watu wangapi walioathirika.

Rejea: Soma kila kitu, Soma kila siku>> https://bbc.in/3jKDTAx

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for