Kuachishwa kazi kwenye makampuni ya teknolojia: Yahoo itapunguza 20% ya wafanyikazi wake.
Kuachishwa kazi kwenye makampuni ya teknolojia: Yahoo itapunguza 20% ya wafanyikazi wake.
Yahoo inapanga kupunguza zaidi ya 20% ya jumla ya wafanyikazi wake 8,600 kama sehemu ya marekebisho makubwa ya kikampuni.
Kampuni hiyo ya kitaalamu ya teknolojia inapanga upya kitengo chake cha utangazaji, ambacho kitapoteza zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa idara hiyo kufikia mwisho wa mwaka.
Takriban wafanyikazi 1,000 wataathiriwa na punguzo hilo kufikia mwisho wa wiki.
Yahoo ndiyo kampuni ya kiteknolojia ambayo imetangaza hasara za kazi huku makampuni mengine yakipambana na kushuka kwa mahitaji(thamani), mfumuko wa bei wa juu na viwango vya juu vya riba.
"Maamuzi haya si rahisi kamwe, lakini tunaamini kuwa mabadiliko haya yatarahisisha na kuimarisha biashara yetu ya utangazaji kwa muda mrefu, huku kuwezesha Yahoo kutoa thamani bora kwa wateja na washirika wetu," msemaji aliiambia BBC.
Yahoo, ambayo imekuwa ikimilikiwa na kampuni ya binafsi ya Apollo Global Management tangu kununuliwa kwa $5bn mwaka juzi(2021), iliongeza kuwa hatua hiyo itawezesha kampuni hiyo kuongeza jitihada zake na kujiwekeza zaidi kwenye biashara yake kuu ya matangazo inayoitwa DSP(Demand-side platform).
Mabadiliko ya utangazaji
Watu kuachishwa kazi ni sehemu ya juhudi pana za kampuni ili kurahisisha shughuli katika kitengo cha utangazaji cha Yahoo.
Limejitokeza hilo baada ya watangazaji wengi kurekesbisha bajeti zao za uuzaji ili kukabiliana na viwango vya juu vya mfumuko wa bei na kuendelea kutokuwa na uhakika juu ya kushuka kwa uchumi.
Kuangaza upya kunalenga nia ya kampuni ya kuacha kushindana moja kwa moja na washindani wake kama Google na Meta ya Facebook kwenye huduma za kimtandao za kutawala matangazo ya kidijitali.
Msemaji wa Yahoo aliongeza: "Jukwaa lao jipya la matangazo litaitwa – ‘Yahoo Advertising’.
"Katika kuongeza juhudi zetu kwenye DSP kwa misingi ya kila kituo, tutatanguliza msaada kwa wateja wetu wakuu duniani, tutazindua tena timu maalum za mauzo ya matangazo ya kidigitali ambao wataelekeza nguvu nyingi kwenye mali(projects) zinazomilikiwa na kuendeshwa na Yahoo - ikiwa ni pamoja na Yahoo Finance, Yahoo News, Yahoo Sports na zaidi."
Rejea kwa Habari Zaidi>>> https://bbc.in/3S2jyU3