Najuta! Kwa Nini Sikuijua Hii Mbinu Mapema.

Najuta! Kwa Nini Sikuijua Hii Mbinu Mapema.

Siku moja nilikuwa naperuzi mtandaoni, ghafla nikakutana na andiko lilokuwa na kichwa cha habari kilichosema: “Wanyama 10 ambao huwezi kuamini kama walikuwepo”

Niliingiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua, ni wanyama gani hasa na umri huu niliokuwa nao, siwezi kuamini kama walikuwepo, mbona kama wanyama wote naamini kama walikuwepo.

Hamu hiyo ilinifanya nilifungue lile andiko na kuendelea kulisoma mpaka mwisho.

Kumbe bhana! Lile andiko halikuwa tu ni andiko la kawaida bali ni tangazo la bidhaa za vitabu vya watoto wadogo.

Sikukubali, nikaamua kufanya utafiti mdogo wa kujua ni nini haswa kilichonifanya mimi kusoma lile andiko mpaka mwisho. Nilichokigundua huwezi amini nitakueleza hapo chini.

Mwandishi wa tangazo lile alitumia njia ya kutengeneza ‘curiosity’ katika kichwa cha habari cha tangazo lake, na njia hiyo waandishi nguli wa matangazo hutumia ili kuteka umakini wa msomaji na aendelee kusoma.

Kutengeneza ‘curiosity’ maana yake ni kumfanya msomaji wako apate hamu ya kutaka kujua zaidi kile ambacho umemgusia katika kichwa cha habari cha tangazo.

Yaani kwa maana rahisi ni kama unavyo kuwa na hamu ya kukikuna kipele kinachowasha.

Ukitaka kutengeneza ‘curiosity’ kwa urahisi tengeneza Pengo la maarifa (knowledge gap): tumia maneno yanayojenga hisia ya yeye kuona kuna vitu vingi bado havijua na anahitaji kuvifahamu.

Mfano:

Hizi Ndizo Sababu za Kwa nini Watu Wanakuwa Matajiri Ndani ya Muda Mfupi,

Usile Vyakula Hivi Ukiwa Ndani ya Basi la Mkoani,

Huu ni Ukweli Mchungu Kuhusu Wanawake Wanene.

Kikubwa cha kuzingatia, hakikisha unakuwa mkweli, usiandike maneno ya kuvutia halafu hutoi kile ambacho umekiahidi itapoteza uaminifu ambapo pia itakupotezea hadhira.

Kuna lolote umejifunza? Tungependa kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for