Siri ya Kuuza Kitu Chochote Ndani ya Dakika 5

Siri ya Kuuza Kitu Chochote Ndani ya Dakika 5

“Hapana, sihitaji bidhaa yako” ni maneno yaliyopita kwenye masikio yangu kutoka Duka la jirani na nilipo kuwepo.

Ilikuwa majira ya saa saba mchana, kwa namna jua lilivyo kuwa kali unaweza kuchomea hata mahindi (Hahah! natania), kijasho chembamba kinamtoka muuzaji aliyeambiwa maneno yale.

Taratibu nilimsogelea na kumuuliza, nini kilijiri. Ndipo aliponisimulia mchakato mzima wa uuzaji alioutumia kwa mteja yule. 

Kuna kosa kubwa alilifanya, kosa ambalo ndio limenisukuma kuandika andiko hili.

Muuzaji alikuwa anataka kumuuzia mteja wake kwa namna yoyote ile, alijiangalia zaidi kuhusu yeye na anachokiuza kuliko kuangalia bidhaa yake inaenda kutatua matatizo ya mteja kiasi gani.

Ikumbukwe kuwa, watu wengi hawapendi kuuziwa bali wanapenda kununua, mtu yeyote akihisi kama anataka kuuziwa ni ngumu kununua. 

Huenda ukawa unajiuliza, sasa nitawezaje kumfanya yeye mwenyewe anunue?

Siri kubwa ipo hapa: cheza na hisia zake (emotion). Kuna msemo maarufu wa bwana Zig Ziglar, unasema: “People buy on emotion and justify on logic.”

Maamuzi ya watu kwenye kununua yanafanywa na hisia (emotion), na namna sahihi ya kushika na kucheza na hisia ya mteja ni kushughulika na tatizo lake, changamoto yake au jambo ambalo linamnyima usingizi. 

Halafu muelezee ni kwa namna gani bidhaa au huduma unayotoa inaenda kuwa suluhu kwa lile linalomsibu.

Mfano:

1. Ni rahisi sana kumuuzia mtu six packs, lakini ni ngumu kumuuzia mafunzo (gym training).

2. Ni rahisi sana kumuuzia mtu utamu/burudani, lakini ni ngumu kumuuzia ubuyu.

3. Ni rahisi sana kumuuzia mtu kupendeza/kuheshimiwa, lakini ni ngumu kumuuzia nguo.

4. Ni rahisi sana kumuuzia mtu usalama wa nyumba, lakini ni ngumu kumuuzia CCTV camera.

5. Ni rahisi sana kumuuzia mtu usingizi mnono, lakini ni ngumu kumuuzia godoro/mto/shuka.

Wewe unauza nini? Tungependa kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

#oasistechtz #oasistechnologiestz

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for