Mbinu Walizotumia Nike Kuteka Soko la Viatu Duniani

Mbinu Walizotumia Nike Kuteka Soko la Viatu Duniani

Historia iliandikwa rasmi mwaka 1964, ambapo kijana mtanashati Phil Knight ambaye alikuwa ni mwanafunzi katika chuo cha Oregon akishirikiana na Bill Bowerman ambaye alikuwa ni mkufunzi na mbunifu wa viatu.

Hawa wote wawili ndio waanzilishi wa Blue Ribbon Sports. Jina kama geni hivi, hapana sio geni kampuni hiyo baadaye ndio iliitwa Nike Inc. Kichwani mwako ukisikia Nike nini kinakuja? Kama sio viatu viatu, ni nini?

Awali kampuni hii ilikuwa ikiagiza viatu kutoka kwenye kampuni iitwayo Onitsuka Tiger iliyopo Japan, ambapo kwa mara ya kwanza waliagiza pair 300. Lakini mwaka 1971 kampuni iliamua kuzindua viatu vyao wenyewe vikiwa chini ya kampuni ya Nike na sio Onitsuka Tiger.

Taratibu kampuni ya Nike ilianza kukuwa na kutambulika na watu wengi zaidi na hii ni kutokana na ubunifu wao katika utengenezaji wa viatu, walitoa aina mbalimbali za viatu vikiwemo: Nike Cortez (1972), Waffle Trainer (1974) na Nike Air (1979).

Pamoja na changamoto nyingi ambazo walikutana nazo ikiwemo ushindani mkubwa wa soko la viatu kama Adidas na Puma na mabadiliko ya namna ya uuzaji kutoka uuzaji wa kawaida kwenda kwenye uuzaji wa mtandaoni (online shopping), lakini bado kampuni ya Nike iliendelea kubuni na kuboresha huduma zao.

Katika miaka ya 1980s na 1990s, kampuni ya Nike ilikuwa ndio kampuni ya kwanza ya viatu duniani huku ikiwa imefika zaidi ya nchi 190 Duniani.

Mwaka 2021, Nike ilizalisha na kuuza pair Bilioni 22.2, ambapo imewaajiri watu takribani 80,000 kutoka nchi mbalimbali huku ikiwa na mapato ya Dola Bilion 44.538 kwa mwaka 2021. (chanzo: macrotrend) 

Historia ya kampuni hii ni pana mno, lengo langu ni kukuonesha namna gani Nike ilivyoweza kujenga brand yake kwanzia kipindi hiko hadi sasa, na hizi ni baadhi ya njia ambazo wamekuwa wakizitumia kujenga brand yao:

  1. Kuteka Hisia: Nike walikuja na kaulimbiu inayosema “Just Do It” ikiwa na maana we fanya tu, haijalishi una kutana na changamoto gani. Watu wengi walishawishika na kuwa karibu na brand hii ya Nike (Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na kaulimbiu katika kampuni yako, ni somo pana, nitaelezea siku zijazo)

 

  1. Mitandao ya kijamii: Nike wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook na Instagram kutangaza bidhaa zao katika ufundi wa hali ya juu huku wakitengeneza maudhui ya kibunifu yenye kuteka umakini wa hadhira zao.

 

  1. Influencer Marketing: Nike wamekuwa wakiingia ushirika na wanariadha maarufu duniani kama Michael Jordan na LeBron James ili kuwafikia walengwa wao.

 

  1. Ufadhili wa shughuli/Hafla mbalimbali ambazo zinaendana na wao wanachokitoa ili kuwafikia watu wengi zaidi ikiwemo Mashindano ya Kombe la dunia na Olympic.

 

  1. Uuzaji kupitia mtandaoni: Nike wametengeneza Website na App yao ambazo unaweza zitumia kuchagua na kununua bidhaa uitakayo kwa kutumia simu au kompyuta yako kisha unaletewa hadi ulipo. Hiyo imerahisisha mchakato wa mauzo.

 

Natumai nawe una biashara au kampuni yako na ungetamani ifike mbali, imefika wakati sasa wa kutoka kwenye ‘comfort zone’ anza kufanyia ‘marketing’ bidhaa au huduma zako kadri uwezavyo.

Tungependa kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for