Tahadhari: Usiposoma Ujumbe Huu, Utakuwa Umekosa Jambo la Muhimu Sana Mwezi Huu.

Tahadhari: Usiposoma Ujumbe Huu, Utakuwa Umekosa Jambo la Muhimu Sana Mwezi Huu.

Jingle bells, jingle bells, jingle all the way….. ♫♪

Ni sauti iliyosikika kwenye masikio ya watu ikiashiria kuwa Krismasi imewadia. Hiyo ilikuwa mwaka 1974 katika nchi ya Marekani. Bwana mmoja hodari na mwanasosholojia aitwaye Phillip Kunz alifanya tukio moja ambalo limekuja kufunza watu wengi baadaye katika miaka ya 2000s. Unataka kulijua hilo tukio?

Ilikuwa alfajiri na mapema, jua limeanza kutoka kwa mbali, huku sauti za ndege na wadudu zikisikika kwa kupokezana, Phillip aliandaa kadi ambazo aliziandika salamu za Krismasi na jumbe nzuri zenye lengo la kutakiana Sikukuu njema.

Alizituma kadi hizo kwa watu 578, tena watu ambao hawafahamu na wala hao watu hawamfahamu Phillip.

Kwanini Phillip alifanya hivyo? Mbona kama ni kupoteza muda? Hayo maswali hata mimi nilikuwa nayo, mpaka pale nilipokuja kujua lengo lake.

Lengo la Phillip lilikuwa ni kufanya utafiti nini kitatokea kama akituma kadi kwa watu asiowajua, je wataguswa? Na wangapi watamjibu hata kama hawamjui. Tafiti yake hii ilichangia katika kukua kwa kanuni iitwayo ‘law of reciprocity’ (nitakuelezea vizuri hapo chini)

Kabla sijaendelea tujue nini kilitokea baada ya watu 578 kupewa kadi na wasiomjua, cha kustaajabisha watu 117 sawa na 20% walijibu tena wengine walituma barua zenye kurasa zaidi ya tatu wakishukuru na kutaka wamfahamu zaidi kwa ukarimu wake.

Phillip alitupa mwangaza wa kanuni ya ‘reciprocity’ yaani kwa ufupi, kawaida ya watu wengi huwa wanajihisi wenye deni kama wakifanyiwa fadhila/wema/upendeleo na mtu mwengine.

Makampuni makubwa duniani wanatumia kanuni hii kupata wateja, kinachofanyika ni kwamba wanakupa kitu chochote cha thamani bure kwako ili ujihisi ni mwenye deni na ulipe kwa kununua kwao. (Hiyo inatokea tu yenyewe, bila hata kuambiwa)

Kitu cha thamani cha bure kinaweza kuwa: elimu, ushauri, tafiti, tabasamu, uchangamfu, kauli nzuri, kipaumbele na ikiwezekana hata sampuli ya bidhaa yako mfano kama unauza karanga kumpa mtu hata kipande cha kashata aonje kabla hajanunua.

Kama wewe ni mfanyabiashara, mtu wa masoko au mtu wa mauzo basi tumia hii kanuni kwenye biashara yako hakika matokeo utayapata.

Tungependa kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for