Jambo Hili Linaweza Kukugharimu Mamilioni ya Fedha

Jambo Hili Linaweza Kukugharimu Mamilioni ya Fedha

Ilikuwa tarehe 10/08/2022 (mwaka jana tu hapo), Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni iliamuru Kampuni ya udalali ya Dexter Insurance kumlipa dereva wa Kampuni ya New Force, Waubani Linyama maarufu kwa jina la 'Ndugu abiria', fidia ya Tsh 150 milioni kwa kosa la kutumia picha yake kibiashara bila idhini yake.

Utakumbuka pia Waubani Linyama ni yule dereva ambaye picha yake ilisambaa akiwa ameshika kipazasauti ndani ya gari alitrend kwa jina la 'Ndugu abiria', watu wengi walitumia picha yake kama meme lakini kampuni ya Dexter Insurance iliangukia kwenye mikono yake na kudaiwa kulipa fidia ya Tsh 150 Milioni.

Kosa hili wengi hulifanya kwa sababu ya mazoea, kutumia kazi za watu wengine ikiwemo picha bila ruhusa zao, unaweza kuta mtu anaenda kwenye Akaunti ya Instagram ya mtu kisha anachukua kazi zake halafu anazifanya kuwa zake bila ya hurusa lakini bila ya kusema chanzo cha hayo maudhui (kutoa credit), kumbuka kufanya hivyo ni makosa na unaweza kuwajibishwa kupitia ‘Intellectual Property Right’ 

Kwa kulijua hilo basi, leo nimekuletea tovuti saba (7) ambazo unaweza pata picha zenye ubora wa hali ya juu bure kisha ukazitumia katika maswala yako ya biashara na ukajiweka katika upande salama.

  1. www.unsplash.com
  2. www.pexels.com
  3. www.pixabay.com
  4. www.stockvault.net
  5. www.picjumbo.com
  6. www.burst.shopify.com
  7. www.freeimages.com

Tungependa kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for