Jinsi ya Kumfanya Mteja Afanye Maamuzi Ndani ya Dakika Tano

Jinsi ya Kumfanya Mteja Afanye Maamuzi Ndani ya Dakika Tano

Umedamka zako asubuhi na mapema, unakimbilia simu yako kabla hata ya kupiga mswaki ili uangalie kama utakuta ujumbe wowote wa ‘good morning’, matokeo yake unakutana na jumbe za matangazo ya mitandao ya simu. Unaamua kwenda WhatsApp Status kuangalia yaliyojiri, ghafla unakutana na wafanya bishara wawili wame’post’ matangazo yao.

Wa kwanza anasema: mzigo mpya wa kutosha wa viatu umeingia, bei nafuu kama unahitaji nitumie ujumbe.

Wa pili anasema: mzigo mpya wa viatu umeingia, zimekuja jozi (pair) 50 lakini zimegombewa sana, zimebaki pair 5 tu, tuma ujumbe sasa hivi kabla nazo hazijaisha.

Ukiwa wewe ni mhitaji wa viatu, yupi ambaye angeweza kuteka hisia yako na kukufanya maamuzi muda huo huo? Bila shaka ni mtu wa pili, unajua kwa nini?

Unapoandika tangazo lako hakikisha ndani yake umeweka ‘hali ya uhaba na uharaka’ ili kumshawishi mteja wako afanye maamuzi bila kuchelewa kwa kumtengenezea kitu kinachoitwa ‘fear of missing out’ (FOMO) hofu ya kukosa, saikolojia inasema watu wengi wanapenda vitu ambavyo wengine wengi wanavihitaji au vipo kwa uchache.

Kuna namna 15 za kutengeneza hali ya uhaba na uharaka katika tangazo lako, lakini leo nitakupa tatu tu (siku zijazo nitamalizia)

1. Onesha bidhaa/huduma zako zimebaki ngapi au kwa watu wangapi. Tumia lugha inayoibua hisia ya uhaba. Mfano, zimebaki nafasi 3 tu ofa hii iishe au pilipili chupa 10 tu pekee kati ya 200 nilizotengeneza wiki hii ndio zimebaki..

2. Weka muda ambao ofa yako itaisha (deadline) mfano Ofa hii itaisha ndani ya masaa 6 yajayo, wote watakaopangisha chumba siku ya leo ‘valentine day’ pekee watapatiwa kifunguakinywa bure.

3. Tengeneza hali ya upekee (exclusivity) yaani hiyo ofa yako inawahusu watu gani wapekee. Mfano, Watu 7 tu wa mwanzo ndio watapata hili punguzo la asilimia 40.

 

Fanya hivi sasa; andika tangazo lako kama kawaida halafu mwisho tengeneza hali ya ‘uharaka na uhaba’ kama nilivyoelezea juu kisha uone matokeo yake, mimi nimekaa paleee.. utanipa mrejesho.

Tungependa kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for