Usikubali 2023 Ufike Mbali Kabla Hujamiliki Tovuti (Website) Yako

Usikubali 2023 Ufike Mbali Kabla Hujamiliki Tovuti (Website) Yako

Kuna kasumba ambayo ipo kwenye vichwa vya watanzania wengi, kuamini kuwa ili umiliki website basi mpaka uwe na biashara au kampuni kubwa, na hapa ndipo walipoendelea wanapotuzidi.

Hivi ni mara ngapi umeenda kwenye Instagram au Facebook ya biashara fulani lakini ukapata tabu kutafuta bidhaa unayoitaka na mwisho wa siku kuachana nayo ni kwa sababu hakuna mpangilio mzuri, hivyo basi faida ya kwanza ya kuwa na tovuti ni kuwa na mpangilio mzuri wa huduma unazozitoa, mteja wako atakipata kitu anachohitaji kwa uharaka sana. Lakini si hivyo tu, zifuatazo ni baadhi ya faida zengine za kuwa na tovuti:

  1. Uaminifu: ukiwa na website, ni rahisi kuaminika na watu na kukuona upo professional na upo serious na unachokifanya.

 

  1. Udhibiti: website inakupa udhibiti kamili kwanzia muonekano na mpangilio wake, ukilinganisha na kwenye mitandao mengine kama instagram udhibiti haupo mikononi mwako upo kwa watu wengine na wana maamuzi ya hata kukufungia bila ya kukupa sababu.

 

  1. Urahisi: kupitia tovuti kunamrahisishia mteja wako kupata taarifa za bidhaa zako na mawasiliano yako kwa urahisi na hata kufanya manunuzi hapo hapo itategemea na aina ya biashara yako.

 

  1. Ni rahisi kufikiwa: mtu akienda google kukutafuta au akienda kutafuta bidhaa ambayo wewe unatoa ni rahisi mno kukupata wewe kama ukiwa na website kupitia search engine optimization (SEO)

 

Hadi hapo natumai utakuwa umeona umuhimu wa kuwa na website. Sasa, unaweza ukawa unajiuliza ntapata wapi hiyo website.

Website zinatengenezwa na watu wenye ujuzi wa maswala ya programming language lakini habari njema ni kwamba Oasis Technologies tumedhamiria kuwasaidia wajasiriamali wadogo kumiliki tovuti zao, tutafute tutakusaidia.

Tunahitaji kusikia maoni yako kuhusu hili, pia usisahau kutufollow katika mitandao yetu ya kijamii (oasis_tech_tz)

About us

Do you believe that your brand needs help from a creative team? Contact us to start working for your project!

Read More

Banner ad

 

Are you looking for